Wagonga nyundo wa London West Ham
United imewatupa nje Majogoo wa Anfield Liverpool katika mchezo wa
raundi ya nne ya kombe la FA.
West Ham walianza kuandika bao lao
la kwanza kupitia kwa Michail Antonio katika dakika ya 45 ya kipindi cha
kwanza baada ya kunganisha krosi nzuri Enner Valencia'sLiverpool wakachomoa bao hilo kupitia kwa kiungo Philippe Coutinho aliyepiga mpira wa adhabu na kujaa nyavuni moja kwa moja.
Dakika tisini zikamalizika kwa sare ya bao 1-1, katika dakika 30, za nyongeza West Ham wakapata bao kupita kwa Angelo Ogbonna,
West Ham watawavaa Blackburn ugenini katika mchezo wa raundi ya tano ya michuano hiyo hapo Februari 21.
No comments:
Post a Comment