Michuano ya klabu bingwa barani
Ulaya imeendelea tena usiku wa Jumatano kwa michezo miwili , Ambapo
Klabu ya soka ya Manchester city imefanikiwa kuchomoza na ushindi mnono
wa magoli 3-1 dhidi ya Dynamo Kiev .
Magoli ya Manchester city
katika mchezo huo yamefungwa na wachezaji Sergio Aguero dk15 , David
Silva dk 40, huku bao la tatu likifungwa na Yahya Touré dk 90.Kwa upande wa Dynamo Kiev bao lao la kufutia machozi limefungwa na Vital Buyal-sky dk 58
Katika mchezo mwingine Psv Eindhovein wakiwa nyumbani wametoshana nguvu na Atletico Madrid kufuatia sare tasa ya bila kufungana.
Michuano hiyo itaendelea tena March 8, 2016 kwa mechi mbili ambapo Real Madrid itaikaribisha Fc Roma na VfL Wolf- Sburg ikichuana na KAA Gent.
No comments:
Post a Comment