Mwanamasumbwi Manny Pacquiao
amelazimika kuomba radhi kutokana na upinzani mkubwa alioupata kutoka
kwa wale wanaounga mkono uhusiano ya jinsia moja.
Sakata hili
limeanza pale ambapo Pacquaio ambaye pia ni mbunge huko kwao ufilipino
aliposema kupitia televisheni kuwa matendo ya jinsia moja ni mabaya
kuliko ya wanyama.Mwanandondi huyo alisema, kwa akili ya kawaida hata wanyama wanajua huyu dume huyu jike, mnyama dume hampandi mnyama dume na jike hampandi mnyama jike, kwa hivyo wanadamu tukiruhusu uhusiano wa jinsia moja basi tunafanya matendo mabaya kuliko hata hao wanyama.
Watu walipomzonga sana, akaweka mtandaoni , picha yake akiwa na mkewe, sasa wamemzonga zaidi kawaomba msamaha lakini akawaambia nimeusema ukweli kama ulivyo kwenye misahafu, Mungu awabariki na ninawaombea
No comments:
Post a Comment