Klabu ya PSG kutoka Ufaransa imepata
ushindi dhidi ya Chelsea mechi ya mkondo wa kwanza Ligi ya Klabu Bingwa
Ulaya huku Benfica nao wakilaza Zenit St-Petersburg.
Bao pekee la Benfica, waliokuwa nyumbani, lilifungwa na Jonas muda wa ziada kutokana na mkwaju wa adhabu uliopigwa na Nicolas Gaitan. Hilo ndilo bao lake la 25 msimu huu na la 45 kufungia Benfica katika mechi 56 tangu alipojiunga nao akitokea Valencia mwaka 2014.
Zenit walisalia wachezaji kumi uwanjani baada ya Domenico Criscito kupewa kadi ya pili ya njano dakika ya 90. Katika ligi Championship nchini Uingereza, Blackburn Rovers walishinda 3-0 dhidi ya Fulham nao Hull City wakatoka sare 0-0 na Brighton & Hove Albion.
No comments:
Post a Comment