Robo fainali nyingine, Chelsea itaifuata Everton katika Robo Uwanja wa Goodison Park, kufuatia kuitoa Manchester City kwa kuifunga mabao 5-1 usiku wa leo Uwanja wa Stamford Bridge, London.
Crystal Palace ya mshambuliaji wa Togo, Emmanuel Adebayor itasafiri kuifuata Reading baada ya kuitoa Tottenham Hotspur leo kwa kuifunga 1-0 Uwanja wa White Hart Lane.
Watford itasafiri kuifuata Arsenal au Hull City, wakati West Ham United itasafiri kuifuata Shrewsbury Town au Manchester United.
Arsenal watarudiana na Hull City kusaka timu ya kwenda Robo Fainali, baada ya sare ya 0-0 Uwanja wa Emirates jana, wakati Shrewsbury Town wataikaribisha Manchester United kesho Uwanja wa New Meadow kuanzia Saa 4:45 usiku.
Mechi za Robo Fainali za Kombe la FA zitachezwa wikiendi ya Machi 11 na 14 mwaka huu.
PICHA
No comments:
Post a Comment