January 9 klabu ya Real Madrid ya Hispania ikiwa na kocha wake mpya Zinedine Zidane katika mchezo wake wa kwanza wa Ligi Kuu Hispania chini ya kocha huyo, imeibuka na ushindi wa jumla ya goli 5-0 dhidi ya Deportivo La Coruna katika uwanja wao wa nyumbani Santiago Bernabeu.
Real Madrid wakiwa na
kocha wao huyo mpya, walionekana kujitahidi kucheza mchezo wa kuvutia na
kufanikiwa kuvuna point tatu muhimu kwa magoli ya Karim Benzema dakika ya 15, 90 na kufuatiwa na hat-trick ya Gareth Bale kwa kufunga goli tatu dakika ya 23, 49 na 63. Huu ni ushindi ambao tunaweza sema umemkaribisha Zidane Santiago Bernabeu.
Video ya magoli ya Real Madrid Vs Deportivo La Coruna
No comments:
Post a Comment