03 January, 2016

TIMU YA VPL YAKANUSHA TAARIFA YA KUHAMA UWANJA

VPL-Logo
Uongozi wa juu wa klabu ya Mgambo JKT ya jijini Tanga umekanusha taarifa za kuuhama uwanja wa Mkwakwani baada ya baadhi ya vyombo vya habari kutoa taarifa kwamba klabu hiyo inampango wa kuuhama uwanja huo  ambao unatumiwa na timu tatu za mkoa huo kwa madai kwamba wamekuwa wakifanyiwa hujuma.
uongozi wa wabeba mitutu hao wa jijini Tanga umeeleza kuwa, hauna mpango wa kuhamisha makazi yao kutoka jijini Tanga kwenda wailayani Handeni kama ambavyo imekuwa ikiripotiwa na baadhi ya vyombo vya habari.
Afisa michezo wa maafande wa Mgambo JKT Luten Luaga amesema, taarifa zilizotolewa na afisa jeshi mstaafu ambaye pia ni mwenyekiti wa chama cha mpira wilaya ya Handeni Abdallah Mtanga si za kweli kwasababu moja ya malengo yao ni kuhakikisha timu yao inajenga mahusiano mazuri na timu za African Sports na Coastal Union na wamekuwa wakicheza mechi za kirafiki mara kwa mara kwa ajili ya kuimarisha vikosi vyao.
Awali afisa mstaafu wa jeshi la wananchi alikaririwa na vyombo vya habari akisema kuwa wanampango wa kuihamisha timu ya Mgambo JKT na kuipeleka wilayani Handeni kwasababu timu zinazoshiriki ligi kuu zipo tatu kwenye mkoa wa Tanga hivyo wanataka kukwepa fitna kutoka kwa timu nyingine za mkoa huo.

No comments:

Post a Comment

Samsung kurejesha fedha kwa wanunuzi wa Note 7

KAMPUNI ya Vifaa vya Elektoriniki ya Samsung ya Afrika Mashariki (SEEA) itarejesha fedha kwa wateja wa simu za Note 7, ambao wataweza kuthib...