Makamo wa pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi amesema bajeti
ya uchaguzi wa marudio imeshatengwa na wanachosubiri ni Mwenyekiti wa
Tume ya Uhaguzi Zanzibar (ZEC) atangaze tarehe hiyo ya kufanya
uchaguzi.
Amesema bajeti hiyo haitatofautiana na ile iliyotumika katika uchaguzi
wa Novemba 2015 iliyofikia karibu ya shilingi bilioni saba.
Amekanusha kauli kuwa uchaguzi huo hautafanyika kwa vile matokeo
yanayolazimisha kutangazwa na CUF yameshafutwa kwa mujibu wa sheria
kutokana na kasoro kadhaa zilizojitokeza.
Akizungumza na waandishi wa habari kuhusu maadhimisho ya Miaka 52 ya
Mapinduzi, Balozi Seif amesema mazungumzo yanayoendelea ni ya kuhakiksha
amani inaimarika Zanzibar na si suala la uchaguzi uliofutwa.
Akizungumzia kuhusu maadhimisho ya miaka 52 sherehe za Mapinduzi Balozi
Seif amewabeza wanaosusuia sherehe hizo kwa madia kuwa Rais Zanzibar Dkt
Ali Mohamed Shein kuwa si halali ni upotoshwaji mkubwa.
Amefahamisha kuwa rais huyo yupo kihalali na hata mawaziri wake wote na
watamaliza ukomo wao atakapoapishwa rais mwingine kama ilivyoanishwa
katika kifungu cha 28 (1) a cha Katiba ya Zanzibar ya mwaka 1984 na si
kama inavyeleezewa kuwa ukomo wake umeisha tangu tarehe 2 Novemba.
Tazama video hii kumsikia akiongea na kujibu maswali ya waandishi kuhusu marudio ya uchaguzi Zanzibar.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
Samsung kurejesha fedha kwa wanunuzi wa Note 7
KAMPUNI ya Vifaa vya Elektoriniki ya Samsung ya Afrika Mashariki (SEEA) itarejesha fedha kwa wateja wa simu za Note 7, ambao wataweza kuthib...
-
C9 Records presents STAR by Foby!. Click DOWNLOAD button bellow to download this song.
-
John ana mke ambaye haoni uzuri wa kitu chochote anachofanya, akifika tu nyumbani mke wake huanza kumlalamika kuwa hela anayoacha nyumba...
-
Mboga za majani na matunda zimekuwa zikisisitizwa kwa sana na wataalamu wa afya hasa kwa wanawake wajawaziti kwani zimekuwa zikiongeza Damu...
No comments:
Post a Comment