08 January, 2016

Trump alidhani mji wa Paris uko Ujerumani?

Trump
Muda mfupi baada ya mwanamume mmoja kuuawa na polisi siku ya maadhimisho ya mwaka mmoja tangu kutokea kwa mashambulio ya Charlie Hebdo nchini Ufaransa, Donald Trump alikuwa anavuma mtandao wa Twitter.
Hii ni kutokana na ujumbe aliouandika kuhusu mashambulio hayo.
Kwenye ujumbe huo, Trump, anayeongoza miongoni mwa wanaotaka kuwania urais Marekani kupitia chama cha Republican, alizungumzia mji wa Paris na nchi ya Ujerumani.
Baadhi ya waliosoma ujumbe huo walionekana kuamini alikuwa akiashiria kwamba mji wa Paris unapatikana Ujerumani.
Vitambulisha mada “Germany is a mess,” (Ujerumani imo matatani) na “Paris is in Germany” (Paris imo Ujerumani) maeneo mengi duniani duniani.
Lakini, mtu anayetaka kuwa rais wa Marekani anaweza kuchanganyikiwa kiasi cha kudhani Paris, mji mkuu wa Ufaransa, unapatikana Ujerumani?
Huku akiendelea kushutumiwa, baadhi waliamini ujumbe wake ulikuwa sahihi na waliokuwa wakimshutumu ndio waliokuwa wamekosea.
Kilichokanganya walioamini kwamba Trump alidhani Paris imo Ujerumani ni hatua yake ya kuzungumzia matukio mawili katika ujumbe mmoja.
Kwenye sentensi yake ya tatu, wanasema, alikuwa anazungumzia matukio mjini Cologne mkesha wa Mwaka Mpya ambapo wanawake karibu 90 wanadaiwa kunyanyaswa kingono.
Waliotekeleza uhalidu huo wanadaiwa kuwa wa asili ya Afrika Kaskazini au Uarabuni. Kumbuka mji wa Munich pia ulikuwa umekumbwa na tishio la shambulio la kigaidi.
Bw Trump amekuwa akishutumiwa vikali, hasa tangu apendekeze Waislamu wazuiwe kuingia Marekani baada ya wanandoa wawili Waislamu kuua watu 14 eneo la San Bernardino, jimbo la California.
Mwanamume aliyeuawa Paris jana anadaiwa kusema ‘Allahu Akbar’ (Mungu ni Mkubwa) nje ya kituo cha polisi eneo la Goutte d’Or karibu na Montmartre, kabla ya kupigwa risasi na polisi.

CHANZO: BBC

No comments:

Post a Comment

Samsung kurejesha fedha kwa wanunuzi wa Note 7

KAMPUNI ya Vifaa vya Elektoriniki ya Samsung ya Afrika Mashariki (SEEA) itarejesha fedha kwa wateja wa simu za Note 7, ambao wataweza kuthib...