14 January, 2016

Timu ya Ura ya Uganda imetwaa ubingwa wa michuno ya mapinduzi kwa msimu wa 2016 kwa kuichapa mtibwa, mabao 3-1.


Watoza kodi wa Ura walianza kuandika bao la kwanza kupitia Julius Ntambi aliyeunganisha mpira wa krosi na goli hilo kudumu mpaka kipindi cha kwanza kinamalizika.
Katika kipindi cha pili timu hiyo ikaongeza mabao mengine mawili kupitia kwa Peter Lwasa katika dakika ya 85 lingine dakika ya 88 akimalizia pasi ya Julius Ntambi na kuwahakishia ubingwa.
Jaffar Salum aliifungia timu yake ya Mtibwa bao pekee la kufutia machozi. Hivyo kuifanya Ura kuondoka na kitita cha Sh. Milioni 10, na kuwa timu ya pili ya Uganda kutwaa taji hilo, baada ya KCCA mwaka 2014.

No comments:

Post a Comment

Samsung kurejesha fedha kwa wanunuzi wa Note 7

KAMPUNI ya Vifaa vya Elektoriniki ya Samsung ya Afrika Mashariki (SEEA) itarejesha fedha kwa wateja wa simu za Note 7, ambao wataweza kuthib...