Majogoo wa Anfield Liverpool wakiwa
katika dimba lao walifunga bao la dakika za mwisho na kulazimisha sare
mechi kati yao na Arsenal, huku Chelsea na Man City pia wakiambulia sare
mechi zao.
Bao la dakika za mwisho la kiungo Joe Allen, ndio
lilowakoa Liverpool baada ya Arsenal kuongoza kwa mabao matatu mpaka
dakika ya 89.Mabao ya Arsenal yalifungwa na Olivier Giroud aliyefunga mawili na Aaron Ramsey akifunga moja huku mabao hayo mengine mawili ya Liverpool yakifungwa na Mbrazil Roberto Firmino.
Chelsea nao waliendela na mwendo wa kuchechemea kwa kukubali sare ya mabao 2-2 na West Bromwich Albion mabao ya Chelsea yakifungwa na César Azpilicueta na Gareth McAuley, beki wa West Brom aliyejifunga, huku West Brom wakipata mabao yao kupitia kwa Craig Gardner na James McClean.
Mabingwa watetezi Manchester City nao wakiwa nyumbani Etihad waliambulia sare ya 0-0 dhidi ya Everton.
Matokeo kamili ya mechi zilizochezwa usiku:
- Chelsea 2 - 2 West Brom
- Man City 0 - 0 Everton
- Southampton 2 - 0 Watford
- Stoke 3 - 1 Norwich
- Swansea 2 - 4 Sunderland
- Liverpool 3 - 3 Arsenal
- Tottenham 0 - 1 Leicester
Nambari | Klabu | Mechi | Mabao | Alama |
1 | Arsenal | 21 | 16 | 43 |
2 | Leicester | 21 | 13 | 43 |
3 | Man City | 21 | 18 | 40 |
4 | Tottenham | 21 | 17 | 36 |
5 | West Ham | 21 | 9 | 35 |
6 | Man Utd | 21 | 7 | 34 |
7 | Stoke | 21 | 2 | 32 |
8 | Crystal Palace | 21 | 3 | 31 |
9 | Liverpool | 21 | -2 | 31 |
10 | Watford | 21 | 1 | 29 |
11 | Everton | 21 | 7 | 28 |
12 | Southampton | 21 | 4 | 27 |
13 | West Brom | 21 | 15 | 27 |
14 | Chelsea | 21 | -3 | 24 |
15 | Norwich | 21 | -11 | 23 |
16 | Bournemouth | 21 | -14 | 21 |
17 | Swansea | 21 | -11 | 19 |
18 | Sunderland | 21 | -15 | 18 |
19 | Newcastle | 21 | -16 | 18 |
20 | Aston Villa | 21 | -20 | 11 |
No comments:
Post a Comment