Barani Ukaya kwasasa ni vurugu kwenye soko la usajili wa wachezaji kila timu ikitaka kujiimarisha kuhakikisha inafanya vizuri kwenye ligi na kumaliza ikiwa imetimiza malengo iliyojiwekea kabla ya kuanza kwa msimu.
Hizi ni story tano ambazo zimepewa kipaumbele kwenye vyombo vya habari vya barani Ulaya.
5. Liverpool imefeli kukamilisha dili la Teixeira
Liverpool imeripotiwa
kurudi nyuma kwenye harakati zake za kuiwania saini ya mshambuliaji wa
Shakhtar Donetsk Alex Teixeira mwenye miaka 26 kutokana na klabu yake
kuihitaji huduma ya mchezaji huyo.
Mchezaji huyo wa kimataifa wa Brazil ambaye ataigharimu Liverpool £28m ameshafunga mabao 26 hadi sasa kwenye michezo 25 ya mashindano yote. (Daily Mail)
4. Newcastle inamtaka Remmy wa Chelea
Striker wa Chelsea Loic Remmy huenda akarejea kwenye klabu yake ya zamani Newcastle United lakini dili hilo litafanikiwa endapo Guus Hidink ataweza kufanikisha kumsajili mshambuliaji wa kibrazil Alexandre Pato.
Mfaransa huyo amejikuta akipambana kuwania nafasi kwenye kikosi cha kwanza cha Stamford Bridge bila mafanikio tangu alipojiunga na mabingwa watetezi wa Premier League akitokea St James Park. (Sources-Chronicle)
3. Beki wa Arsenal anataka kuondoka
Arsenal huenda ikampoteza beki wake Mathieu Debuchy kwenye kipindi hiki cha usajili wa dirisha dogo kutokana na beki huyo kuwaniwa na vilabu vya Sunderland na AstonVilla.
Mchezaji huyo wa kimataifa wa Ufaransa alijiunga na Arsenal akitokea Newcastle United lakini nafasi yake kwenye kikosi cha kwanza imechukuliwa na Mhispania Hector Bellerin.
Michuano ya Euro inakaribia kuanza na endapo ataendelea kusugua benchi atapoteza nafasi kwenye kikosi cha Ufaransa ambao ndiyo waandaaji wa michuano hiyo.
Anatafuta nafasi ya kwenda kucheza kwa mkopo kwenye kikosi cha Aston Villa lakini boss wa Sunderland Big Sam naye pia anamuwinda. (Source: The Daily Mail)
2. Kwasasa siko tayari kujiunga na Man United
Taarifa ambazo hazijathibishwa kutoka Hispania zinadai kwamba, mshambuliji wa Real Madrid Gareth Bale angejiunga na Manchester United lakini kukosekana kwa mfululizo wa matokeo mazuri kwenye klabu hiyo kumemfanya abadili maamuzi. (Source: The Independent)
1. Ed Woodward amshauri Van Gaal kusalia United
Gazeti la The Sun la Uingereza limesema kwamba, Manager wa Manchester United Louis Van Gaal aliomba kujiuzulu baada ya kipigo cha Jumamosi iliyopita kutoka kwa Southampton lakini aliombwa kuendelea kusalia United na makamu mwenyekiti wa timu hiyo Ed Woodward ambaye hataki kubadili kocha katikati ya msimu. (Source: The Sun)
No comments:
Post a Comment