Mshambuliaji wa ‘wekundu wa Msimbazi’ Simba Ibrahim Ajib ametangazwa kuwa mchezaji bora wa mwezi December wa klabu hiyo.
Ajib amefanikiwa kunyakua tuzo hiyo baada ya kufanikiwa kufanya vizuri kwenye mechi za mwezi December, 2015 ambazo zimemfanya apate kura nyingi katika kinyang’anyiro hicho.
Simba ndiyo klabu pekee ya VPL yenye utaratibu wa kutoa tuzo ya mchezaji bora kila mwaka. Mshindi wa tuzo hiyo hupatikana kwa kupigiwa kura na wanachama wa klabu hiyo.
Hamis Kiiza na Mohamed Hussein ‘Tshabalala’ wameshatwaa tuzo hiyo ambapo Ajib ameungana nao katika orodha hiyo ya wachezaji ambao tayari wameshafanikiwa kutwaa tuzo ya mchezaji bora wa mwezi
No comments:
Post a Comment