19 January, 2016

NIGERIA WAWAFUMUA 4-1 NIGER CHAN 2016,

TIMU ya taifa ya Nigeria imeanza vyema Michuano ya Ubingwa wa Mataifa ya Afrika (CHAN), inayohusisha wachezaji wanaocheza ligi za nchini mwao pekee, baada ya kuwafunga jirani zao wa Magharibi mwa bara, Niger mabao 4-1 katika mchezo wa Kundi C leo Uwanja wa Nyamirambo mjini Kagali.
Washindi hao wa Medali ya Shaba katika fainali za mwaka 2014 zilizofanyika nchini Afrika Kusini, walitawala kipindi cha kwanza, lakini hawakufanikiwa kupata bao.


Lakini kipindi cha pili mambo yakawanyookea na ndani ya sekunde 30 Osas Okoro akawafungia Tai hao bao kwa kwanza, kabla ya Chisom Chikatara kufunga mara tatu mfululizo, dakika za 75, 82 na 90.
Nigeria sasa inaongoza Kundi C, baada ya Tunisia kutoa sare ya 2-2 na Guinea katika mchezo uliotangulia wa kundi hilo. Mabao ya Tunisia yamefungwa na Ahmed Akaichi dakika ya 33 na 51, wakati ya Guinea yamefungwa na Alseny Camara Agogo dakika ya 40 na 83.

No comments:

Post a Comment

Samsung kurejesha fedha kwa wanunuzi wa Note 7

KAMPUNI ya Vifaa vya Elektoriniki ya Samsung ya Afrika Mashariki (SEEA) itarejesha fedha kwa wateja wa simu za Note 7, ambao wataweza kuthib...