Umoja wa mataifa umesema kuwa
misafara ya magari iliyobeba chakula cha mwezi mzima na dawa leo umeanza
kuelekea nchini Syria katika mji wa Madaya eneo ambalo limeathiriwa na
njaa ambapo baadhi yao wamekufa kutoka na hali hiyo.
Watu zaidi ya
elfu 40 wamezuiwa na serikali kutoka katika maeneo hayo na hawajahi
kupokea msaada wa chakula tangu mwezi Oktoba mwakajana.UN wanasema kuwa wanaushahidi kwamba baadhi wamekufa kwa njaa katika mji huo wa Madaya nchini Syria kutokana na msimamo wa serikali kutoruhusu mashirika ya misaada kuingi eneo hilo kutokana na mapigano.
Wiki iliyopita serikali ya Syria imeruhusu misafara ya mashirika ya misaada kuingia kuingia katika eneo.Msemaji wa umoja wa mataifa vikwazo vya kiutawala kwa sasa vimetatuliwa pia.
Misaada hiyo itapelekwa kwa serikali za vijiji viwili vya jimbo la Idlib vinavyokaliwa na waasi.
No comments:
Post a Comment