Kundi la wapiganaji wa Kiislamu la
al-Shabab kutoka Somalia limetoa kanda ya video ya propaganda ambapo
wanamtaja mgombea urais wa Marekani Donald Trump.
Hii imejiri wiki
kadha baada ya Trump, anayeongoza kinyang’anyiro cha kutafuta
atakayepeperusha bendera ya chama cha Republican, kupendekeza
Waislamu wazuiwe kuingia Marekani.Kundi la al-Shabab, ambalo lina uhusiano na mtandao wa Al-Qaeda, linaelekeza ujumbe kwa Wamarekani weusi, likiwahimiza kusilimu na kushiriki kwenye Jihad au vita vitakatifu.
Kundi hilo linasema kwenye video hiyo kwamba ubaguzi wa rangi, ukatili wa polisi na chuki dhidi ya Waislamu vimesheheni Marekani.
Wasimamizi wa kampeni ya Bw Trump hawajazungumza lolote kuhusu video hiyo.
Miaka ya hivi karibuni, Wasomali-Wamarekani kutoka Minnesota wameripotiwa kwenda Somalia kujiunga na al-Shabab.
No comments:
Post a Comment