Filamu mpya ya Star Wars ya The Force Awakens ndiyo iliyovuma zaidi Uingereza mwaka 2015, licha ya kuwa sokoni siku 16 pekee.
Filamu hiyo ilipokea mauzo ya tiketi ya £94.06m na kuishinda filamu ya Spectre ambayo ilizoa £93.5m.Filamu hiyo ya JJ Abram pia imeishinda Avatar (£ 94m) ambayo ndiyo iliyokuwa ya pili kwa umaarufu nchini Marekani.
Lakini filamu ya Skyfall bado inang'aa katika historia ya Marekani ikiwa ndiyo iliyovuma zaidi katika historia huko. Filamu hiyo ilipata £103m mwaka 2012.
The Force Awakens imeshirika waigizaji wa kwanza kabisa wa filamu za Star Wars Harrison Ford, Carrie Fisher na Mark Hamill, na pia waigizaji wapya kama vile Waingereza Daisy Ridley na John Boyega.
Mwishoni mwa Desemba, Star Wars: The Force Awakens ilivunja rekodi na kuwa filamu iliyozoa $1bn (£674m) kwa kasi zaidi duniani.
Ilivunja rekodi hiyo kwa kuzoa pesa hizo katika kwa siku kumi na mbili pekee, na kuishinda rekodi ya awali ya siku 13 iliyowekwa na Jurassic World mwezi juni.
Ingawa Jurassic World ilikuwa na nafuu wa kuonyeshwa Uchina pia, filamu ya The Force Awakens bado haijaanza kuonyeshwa huko.
Lakini bado itatumia wakati kabla kukamilisha filamu hizo mbili ambazo zimetumia zaidi ya $2bn ulimwenguni - 1997 Titanic ($2.18bn; £1.45bn)na 2009's Avatar ($2.78bn; £1.85bn)
Filamu hizi mbili zilielekezwa na James Cameron na zilizinduliwa muda mfupi kabla Krismasi sawa na filamu ya The Force Awakens.
No comments:
Post a Comment