21 January, 2016

Djokovic na Serena Williams wasonga

Djokovic
Mabingwa watetezi wa mashindano ya tenisi ya Australian Open Novak Djokovic na Serena Williams wamefuzu kwa raundi ya tatu ya mashindano hayo.
Nyota mwingine Petra Kvitova hata hivyo ameshindwa kufuzu.
Mchezaji nambari moja duniani upande wa wanawake Williams alimtoa raia wa Taiwan Hsieh Su-Wei 6-1 6-2 naye Djokovic akamondoa Mfaransa Quentin Halys kwa kumshinda 6-1 6-2 7-6 (7-3).
Roger Federer na Maria Sharapova pia wamesonga kwenye mashindano hayo yanayoendelea Melbourne.Serena
Lakini bingwa mara mbili wa Wimbledon Kvitova wameshindwa 6-4 6-4 na raia wa Australia Daria Gavrilova mwenye umri wa miaka 21.
Nyota wa Uingereza Andy Murray na Johanna Konta watarejea uwanjani raundi ya pili Alhamisi.

No comments:

Post a Comment

Samsung kurejesha fedha kwa wanunuzi wa Note 7

KAMPUNI ya Vifaa vya Elektoriniki ya Samsung ya Afrika Mashariki (SEEA) itarejesha fedha kwa wateja wa simu za Note 7, ambao wataweza kuthib...