21 January, 2016

2 Chainz atoa msaada wa nyumba kwa familia ya watu 11

Screen-Shot-2016-01-20-at-11.52.19-AM-640x302
2 Chainz anaendelea kuwa mstari wa mbele kwenye kutoa misaada kwa watu tofauti toka mwaka jana. Rapa huyu ambaye ametengeneza zaidi ya milioni kumi kutoka kwenye biashara yake ya masweta ya father X Mass ametoa msaada mwingine mkubwa.
2 Chainz ametoa nyumba yenye vyumba vitano, mabafu mawili kwa familia ya watu 11 isiyokuwa na makazi. Nyumba hii imetolewa kupitia taasisi ya misaada ya 2 Chainz ya TRU.
Msaada huu umetolewa January 19 kwa familia hii yenye watoto mapacha, 2 Chainz aligundua kuhusu familia hii kupitia GoFundMe huduma ya michango ya kanisa la Atlanta. Familia hii ilikuwa inaishi kwenye mazingira mabaya na baba yao alikuwa mgonjwa na kusnindwa kuhudumia familia yake mpaka kanisa lilipoingilia.
2 Chainz anasema “Ni mwanzo wa mwaka na hizi pesa hapa sio sehemu ya kodi zangu, nimuhimu kuweka tabasamu kwenye nyuso za watu ”

No comments:

Post a Comment

Samsung kurejesha fedha kwa wanunuzi wa Note 7

KAMPUNI ya Vifaa vya Elektoriniki ya Samsung ya Afrika Mashariki (SEEA) itarejesha fedha kwa wateja wa simu za Note 7, ambao wataweza kuthib...