08 December, 2015
UJUE UTATA WA JOHN CENA KWA MPENZIWE
Kwa kila mfuatiliaji ama hata yule ambaye sio mfuatiliaji sana wa mieleka maarufu kama WWE (World Wrestling Entertainment) atakua anamfahamu Super Star John Cena. Kwa taarifa yako tu John Cena ni kati ya wanamieleka bora zaidi wa muda wote katika historia ya WWE.
Lakini pamoja na mambo mengi makubwa ya ulingoni aliyokwisha yafanya gwiji huyu, pia ana mahusiano ya kimapenzi na mmoja wa Total Divas anaitwa Nicole maarufu Nicky Bella.
Wawili hao walianza mahusiano yao miaka mitatu iliyopita na kiukweli Cena kakamatika. Sasa pamoja na mambo mengine ya kimahusiano, mchumba wake Nicole amekua akitamani kwa udi na uvumba kupata mtoto kutoka kwa staa huyo wa muda wote katika historia ya mieleka.
Lakini unajua John Cena kajibu nini kwa mpenziwe huyo baada ya kutamani wazae mtoto?? John anadai pamoja na kumpenda sana staa huyo mwenzake wa mieleka lakini hataki kuzaa naye wala kumuoa, anataka mapenzi tu.
Majibu hayo yanamuumiza kichwa Nicole Bella ambaye anatamani kuzaa mtoto lakini mpenziwe hana mpango. Lakini yuko staa mwingine anaitwa Dolph Zigler yeye anamzimia huyu binti na yuko tayari kumfanya mama, lakini Nicole naye anamzimia sana John, tusubiri kuona itakuaje baadae.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
Samsung kurejesha fedha kwa wanunuzi wa Note 7
KAMPUNI ya Vifaa vya Elektoriniki ya Samsung ya Afrika Mashariki (SEEA) itarejesha fedha kwa wateja wa simu za Note 7, ambao wataweza kuthib...
-
C9 Records presents STAR by Foby!. Click DOWNLOAD button bellow to download this song.
-
John ana mke ambaye haoni uzuri wa kitu chochote anachofanya, akifika tu nyumbani mke wake huanza kumlalamika kuwa hela anayoacha nyumba...
-
Mboga za majani na matunda zimekuwa zikisisitizwa kwa sana na wataalamu wa afya hasa kwa wanawake wajawaziti kwani zimekuwa zikiongeza Damu...
No comments:
Post a Comment