Mgombea urais wa chama cha Republican Donald Trump amesema ameahirisha ziara yake aliyopangiwa kuifanya nchini Israel.
Mfanyabiashara huyo tajiri ameandika kwenye Twitter kwamba atafanya ziara hiyo “baadaye baada yangu kuwa Rais wa Marekani”.Mapema wiki hii, Bw Trump alipendekeza Waislamu wazuiwe kwa muda kuingia Marekani.
Tamko lake lilishutumiwa vikali na viongozi duniani, akiwemo Waziri Mkuu wa Israel Benjamin Netanyahu.
Matamshi hayo ya Trump lingetia utata kwenye ziara hiyo upande wa kiongozi huyo wa Israel, ambaye hangetaka kuwaudhi Waislamu.
“[Bw Netanyahu] alisema tutakuwa na mkutano na anasubiri kwa hamu mkutano huo na mengine mengi. Lakini sikutana kumuwekea shinikizo,” Bw Trump aliambia Fox News mnamo Alhamisi.
Pendekezo lake alilitoa baada ya shambulio lililoua watu 14 mji wa San Bernardino, jimbo la California, ambalo lilitekelezwa na wanandoa Waislamu waliokuwa na itikadi kali.
No comments:
Post a Comment