KLABU
ya Manchester United ipo kwenye mazungumzo ya kumsajili kiungo Lazio,
Felipe Anderson katika jitihada zake za kusaka kiungo mbunifu.
Mbrazil
huyo mwenye umri wa miaka 22 alitakiwa na kocha Louis van Gaal tangu
mwanzoni mwa msimu na wasaka vipaji wa Old Trafford wameendelea
kufuatilia maendeleo yake mjini Rome, huku Lazio ikimthaminisha kwa
Pauni Milioni 35.
United
bado inafanya mpango wa kumsajili Sadio Mane - ambao ulikwama Agosti -
na Southampton haiko tayari kumuuza mmoja wa wachezaji wake tegemeo
Januari.
Anderson, ambaye amefunga mabao matano msimu huu kutoka eneo la kiungo, amezivutia klabu nyingine kadhaa kubwa Ulaya.
United
imejikuta katika wakati mgumu msimu huu kutokana na kukosa kiungo wa
maana na inajipanga kuimarisha kikosi chake kabla ya kuanza mzunguko wa
pili wa Ligi Kuu ya England.
No comments:
Post a Comment