14 December, 2015

Director wa Bongo hawathamini kazi za wasanii ndio maana wanakimbilia nje!

post-feature-imageNimeamka leo nakusema niitizame video ya 'Malikia' aliyoimba Kala Jeremiah. Kwangu mimi namkubali sana Kala kwa kazi yake ambaye anaifanya kutokana na mashairi anayoimba yanakuwa yanabeba ujumbe ambao unafaa kwa jamii ya Tanzania na hata wengine wanao elewa lugha ya kiswahili.

Video nimoja ya njia inayoweza kumsababisha mwanamuziki kufika nje kupitia media zilizo nje ya Tanzania na watu wakaipenda mwisho wa siku hata msaniii huyo kupata show ughaibuni.

Video ya Kala imekuwa ya kawaida kama video ambazo tumezizoea ki Bongo bongo kitu ambacho kwasasa Watanzania wamekichoka na wanataka kitu kipya na ubunifu mpya. Msanii anaweza kuja na wazo lake la kimuziki kuwa anataka nini na director akaki convert nakutengeneza kitu amazing.

Lakini kwa video ya Kala Jeremiah director, editor na hata msanii mwenyewe hawajatutendea haki. Katika video ambayo tunasema impe msanii jina heshima sio yakuacha na kuonyesha Drone Camera kwenye video ambayo tunasema ni official, Labda kama ni behind the scene
tutaelewa lakini sio official.
 Soko la muziki wa Bongo limekuwa likilalamikiwa kwa uizi wa kazi za wasanii hadi leo wanaogopa kutoa album, je tutataka life kama tunavoona kwenye soko la filamu Tanzania 'Bongo Movie'? Director na wasanii kagueni kazi na muridhike nayo kabla ya kupeleka kwa jamii hata kama hutaki upate faida kutoka kwa kazi hiyo basi pata heshima!

No comments:

Post a Comment

Samsung kurejesha fedha kwa wanunuzi wa Note 7

KAMPUNI ya Vifaa vya Elektoriniki ya Samsung ya Afrika Mashariki (SEEA) itarejesha fedha kwa wateja wa simu za Note 7, ambao wataweza kuthib...