13 August, 2015

Watu 30 wameuawa Baghdad


Mlipuko mkubwa kutoka kwa lori lililokuwa limeegezwa katika mji mkuu wa Iraq, Baghdad umesababisha vifo vya zaidi ya watu 30.Maafisa walisema kuwa gari lililokuwa na mtambo wa kutengeneza barafu lililipuka Kaskazini Mashariki mwa jiji hilo.

Mlipuko huo ulitokea katika eneo la soko lililo na watu wengi karibu na Wilaya inayokaliwa zaidi ya Washia ya Sadri
Hakuna kundi lolote lilolodai kuhusiana na mlipuko huo.
Wapiganaji wa kundi la Waislamu wenye itikadi kali hushambulia maeneo yanayokaliwa na Washia mara nyingi.
150609233532_baghdad_640x360_ap

No comments:

Post a Comment

Samsung kurejesha fedha kwa wanunuzi wa Note 7

KAMPUNI ya Vifaa vya Elektoriniki ya Samsung ya Afrika Mashariki (SEEA) itarejesha fedha kwa wateja wa simu za Note 7, ambao wataweza kuthib...