Wakimbizi wa kwanza 100 wamerejeshwa
Somalia kufuatia makubaliano kati ya Shirika la Umoja wa mataifa
linaloshughulikia maswala ya wakimbizi,UNHCR na serikali ya Kenya na
Somalia.
Kiongozi wa UNHCR bwana Raouf Mazou anasema kuwa ”huu ni mwanzo mpya””Ndege za kwanza mbili, zimeondoka Daadab kuelekea Kismaayona miji mingine midogo ya Luuq na Baidoa.”Serikali ya Kenya ilikuwa imetishia kuwafurusha wakimbizi wa Somalia kutoka kwenye kambi ya Dadaab kufuatia ripoti za kijasusi zilizoeleza kuwa njama zote za mashambulizi ya Kundi la wapiganaji wa Kiislamu kutoka Somalia,Al Shabaab yalikuwa yakipangwa na kufanikishwa kutoka Dadaab.
Kenya ilitoa amri hiyo punde baada ya wanamgambo wa kiislamu wa Al Shabaab kuwaua wanafunzi wakristu takriban 150 katika chuo kikuu cha Garissa mapema mwezi Aprili.
No comments:
Post a Comment