06 August, 2015

Messi alivyokasirika akampiga kichwa huyu jamaa wa AS Roma.

Mshambuliaji wa kimataifa wa Argentina anaeichezea klabu ya FC Barcelona ya Hispania Lionel Messi alishindwa kuzuia hasira zake baada ya kupigwa kikumbo na Mapou Yanga-Mbiwa wa klabu ya AS Roma ya Italia, tukio hilo lilitokea katika mchezo wa kirafiki ambapo timu zote mbili zilikuwa zinautumia mchezo huo kama sehemu ya maandalizi ya mwanzo wa msimu.
Barcelona-v-Roma
Messi akiwa na hasira alimfuata Yanga-Mbiwa na kumpiga kichwa na mwamuzi aliwaonya kwa kuwaonyesha kadi za manjano wote wawili,mchezo ulimalizika kwa FC Barcelona kushinda kwa jumla ya goli 3-0 magoli ambayo yaliwekwa wavuni na wachezaji Neymer dakika ya 26, Messi dakika ya 41 na Rakitic akaitimisha goli la mwisho dakika ya 66 ya mchezo.
Barcelona's Lionel Messi, right, and Roma’s Mapou Yanga-Mbiwa get involved in a scuffle during the Joan Gamper trophy soccer match between FC Barcelona and AS Roma at the Camp Nou stadium in Barcelona, Spain, Wednesday, Aug. 5, 2015. (AP Photo/Francisco Seco)

messi-yanga-barcelona-roma_1008y8l3pt7911gg6266p37hqu
Nimekusogezea video ya tukio lenyewe

No comments:

Post a Comment

Samsung kurejesha fedha kwa wanunuzi wa Note 7

KAMPUNI ya Vifaa vya Elektoriniki ya Samsung ya Afrika Mashariki (SEEA) itarejesha fedha kwa wateja wa simu za Note 7, ambao wataweza kuthib...