Nyota mpya wa Manchester United, Memphis Depay unaweza kusema amefanya maamuzi magumu ya kuvaa viatu vizito.
Kuelekea msimu ujao wa ligi kuu England unaoanza Jumamosi hii, Depay ameomba kupewa jezi ya heshima Old Trafford, namba 7.
Mshambuliaji
huyo kinda amejitosa kuchukua jezi hiyo ya maana ambayo iliwahi
kuvaliwa na masupastaa wa maana waliowahi kucheza Manchester United
wakiwemo George Best, Bryan Robson, Eric Cantona, David Beckham na
Cristiano Ronaldo na nyota wa sasa anayeondoka, Angel di Maria.
Inafahamika kwamba kocha wa United, Louis van Gaal bado hajatoa namba katika kikosi chake.
Namba 9 pia iko wazi, lakini Van Gaal amevutiwa na maombi ya Depay kwani inaonesha jinsi gani Mholanzi huyo anajiamini.
No comments:
Post a Comment