Mabadiliko si ‘ kitu cha
kuhesabu’, lakini mengi yanatokea. Yoote husababishwa na ‘ Kiu’, ikiwa
Azam FC walikuwa na kiu ya kutwaa ubingwa wa kwanza wa Tanzania Bara,
Simba SC, Yanga SC wao pia walikuwa na kiu ya kutaka kuongeza mafanikio
zaidi ya ndani ya uwanja kwa ushindi wa mataji kila msimu. Kiu si kitu
cha kuburudika au kuondoka, Iliumbwa sababu ya Uhai, na itaondoka sababu
ya uhai. Kiu gani wanayo klabu kubwa kama Simba Sc?
Tuachane na ukweli kuwa klabu hii
( Simba SC) ni mabingwa mara 19 wa Kihistoria wa ligi kuu ya Bara, timu
hiyo kwa sasa imekuwa na –u-haba’ wa mataji ya ligi kuu na kile cha
kusikitisha zaidi kwa wapenzi wa klabu hiyo ni kukosa kuwa miongoni mwa
klabu Mbili za juu kwa msimu mitatu mfululizo. Kiuhalisia nafasi ya
Simba hivi sasa imechukuliwa na Azam FC ambayo ndani ya misimu minne
mfululizo timu hiyo ya Chamanzi imemaliza namba 2 mara tatu na mara moja
wamefanikiwa kushinda ubingwa.
Siku zinapita, lakini Simba
wanaendelea kuhangaikia ‘ Kiu Yao’ ya kurudi miongoni mwa klabu mbili
bora za Bara na hata kushinda ubingwa wa kwanza tangu walipofanya hivyo
mara ya mwisho msimu wa 2011/12. Simba wanashindwa kuiangamiza kiu,
lakini Kiu hiyo imekuwa ikiwaangamiza kwa miaka mitatu mfululizo. Je,
wataishinda Kiu hiyo msimu ujao?
USAJILI……
Achana na usajili ulio mbioni
kukamilika wa wachezaji Mreno, Ricardo de Andrade ambaye ni mchezaji wa
nafasi ya u-golikipa,Mshambulizi Mmali, Makan Dembele, Straika Mrundi,
Kevin Ndayisenga ambao wataungana na Waganda, mlinzi wa kati, Juuko
Murishid, kiungo, Simon Sserunkuma na mshambulizi Hamis Kizza na
Mzimbabwe, Justice Majabvi ambaye ana uwezo wa kucheza nafasi ya ulinzi
na ile ya kiungo.
Nyota hawa saba wa kimataifa
wanatazamwa kwa jicho la ‘ ukombozi’ wakichanganyika na sehemu ya timu
iliyoandaliwa takribani miaka mitatu iliyopita. Katika misimu mitatu ya
mwisho kuelekea msimu wa 2015/16, Simba imefanya usajili wa wachezaji
wengi wa Kimataifa lakini tuseme ukweli ni Emmanuel Okwi pekee ambaye
amejitahidi kuisaidia klabu hiyo, pia mchango binafsi wa mshambulizi
Mrundi, Amis Tambwe msimu wa 2013/14 utaendelea kukumbukwa.
Okwi alikuwa na matatizo ya nje
ya uwanja-Kuchelewa kurejea klabuni kila alipopewa ruhusa ya kwenda kwao
lakini aliporejea na kupewa nafasi ya kucheza alikuwa bora kuliko. Kama
usajili huu Utalipa kwa Simba wanaweza kufanya vizuri na kukata kitu
yao licha ya kwamba hawataimaliza. Nyota wa kimataifa wamekuwa na
mchango mkubwa kwa klabu za Azam FC na Yanga SC katika kipindi cha
misimu mitatu iliyopita lakini kwa Simba wamekosa utulivu na wengi licha
ya kusajiliwa kwa matarajio makubwa hushindwa na kuondoolewa mapema.
NYOTA WAPYA WENYE UZOEFU……
Mashabiki wa Yanga SC wanasema
Musa Hassan Mgosi ni ‘ Mzee’, lakini sivyo, kama Musa atajibidiisha
anaweza kuwa mfungaji bora wa muda woote wag emu za ‘ Dar es Salaam
derby’. Mgosi amekwisha funga mara nne katika mipambano ya Simba na
Yanga na msimu wa mwisho alifunga mara mbili katika ushindi wa Simba 4-2
Yanga, April, 2011. Simba wenyewe hawana shaka kuhusu Musa kwa kuwa
hivi sasa ni mchezaji anayepevuka zaidi kiakili, kiuchezaji na nidhamu.
Kitendo cha kupewa u-nahodha wa
klabu hiyo kwa mara nyingine kitachochoea uwezo wake na ataendelea
kufunga mabao muhimu hata kama hatooshinda tena tuzo ya ufungaji bora
kama alivyofanya misimu mitano iliyopita. Mgosi anaungana na kijana
Daniel Lyanga kama maingizoo mapya ‘ wazawa’ katika safu ya
mashambulizi. Bila shaka wataziba nyufa hizo vizuri sambamba na
washambuaji wapya waliosajiliwa kutoka ng’ambo ya nchi.
Peter Mwalyanzi ni mchezaji wa
nafasi ya kiungo wa mashambulizi, huyu ana uwezo wa kucheza kama wing
pia. Ni mchezaji mwenye kasi na mzuri katika kumiliki mpira, alicheza
vizuri kiasi katika pambano dhidi ya SC Villa ya Uganda siku ya Jumamosi
iliyopita na alionesha kuwa Simba haikukosea kumsaini kutoka Mbeya City
FC. Mlinzi wa kati, Mohamed Fakhi na Yule wa pembeni Samih Hajji Nuhu
pia wameongezwa kuongeza namba ya walinzi.
Usajili huu unaweza kutosheleza
kiu ya klabu, mashabiki na wapenzi?. Chini ya mwalimu raia wa Uingereza,
Dylan Kerry na wasaidizi wake, Suleimani Matola ( koocha msaidizi),
Idd Salim ( kocha wa magolikipa) na mtaalamu wa mazoezi ya viungo,
Mromania, Momeilovic Dusan timu hiyo haitashindwa kirahisi msimu ujao
kwa kuwa utawala umeonekana kuwa makini katika usajili na uboreshaji wa
benchi la ufundi. Nyota wapya na timu mpya ya ufundi wanaweza
kushilikiana vizuri na nyota waliowakutana na kutengeneza ‘ sura ya
matumaini’.
Simba haijakosea kumsaini kwa
mara ya pili kiungo Mwinyi Kazimoto kwa kuwa timu ilihitaji wachezaji
wazoefu wenye uwezo kama Mwinyi, Mgosi, Kizza na wengineo. Nafikiri
Ingizo la Lyanga litageuka kutoka usajili wa kawaida hadi kuwa mchezaji
muhimu. Kwa usajili Simba hawajakosea sana wamejitahidi kwa kiasi cha
kuridhisha.
WACHEZAJI VIJANA……..
MANYIKA Peter Jr, Hassan Kessy,
Mohamed Hussein ‘ Tshabalala’, nahodha msaidizi Hassan Isihaka, Juuko,
Abdi Banda, Said Ndemla, Jonas Mkude, Simon, Ibrahim Ajib ni baadhi ya
wachezaji vijana watakao endelea kuichezea klabu hiyo msimu ujao. Simba
ilisemwa kutokuwa na uzoefu wa wachezaji hao katika ligi kuu ndiyo
kumesababisha washindwe kufanya vyema katika ligi kuu na wao
walichukulia kama sababu ya kuficha udhaifu wa timu ndani ya uwanja.
Je, nyota hawa vijana ambao
wanakwenda kucheza msimu wan ne katika ligi kuu watakuwa wamejifunza na
kujiongezea mbinu na maarifa zaidi ili kuisaidia klabu yao msimu ujao?.
Ibrahim Twaha, Abdallah Seseme, Ramadhani Singano, Okwi, Elius Maguli,
Hussein Sharrif, William Lucian ni baadhi ya vijana ambao wameondooka
klabuni msimu huu ili kupisha wachezaji wapya wenye uzoefu.
Kundi la vijana kina Isihaka ni
lazima sasa wawe na kiu ya kushinda ubingwa wa Tanzania Bara kwa kuwa
kutofanya hivyo msimu ujao klabu itakuwa imekaa kwa miaka minne
mfululizo pasipo kushinda ubingwa huo. Simba iliwahi kusubiri kwa miaka
minne kushinda ubingwa wa kwanza wa ligi kuu. Kati ya 1996 hadi mwaka
2000 timu hiyo ya ‘ Mtaa wa Msimbazi’ iliishi bila kushinda ubingwa wa
ligi.
Sasa hakuna tena kisingio cha
ukosefu wa uzoefu, Simba watapaswa tu kupiga na kushinda moja ya nafasi
mbili za juu na wachezaji vijana wanatakiwa kusahau kuhusu umri wao na
kucheza kwa malengo ya kushinda tu.
HOFU…….
Baada ya kuwaajiri walimu wa
kutosha katika benchi la ufundi, labda sasa utawala unapaswa
kujirekebisha na tatizo lao la mar azote-Kuingilia na kushinikiza
maamuzi yao kwa benchi la ufundi. Makocha wooote wa klabu hiyo wamekuwa
wakilalamikia hali hiyooo mara baada ya kufukuzwa lakini afadhali kwa
Mserbia, Goran Kopunovic ambaye alionekana kuwa huru katika kazi yake.
Simba itafanikiwa kumaliza kiu
mojawapo ( kumaliza nafasi ya pili au kushinda ubingwa) ikiwa tu
wachezaji watajituma, watacheza kwa usikivu na kufuata maelekezo ya
benchi la ufundi. Kiu ya mafanikio imewaganda mashabiki na wapenzi wa
klabi hiyo. Kiu hii itamalizwa kama kila mtu atafanya kazi yake kwa
uhuru, vinginevyo Azam FC na Yanga SC zitaendelea kutawala nafasi mbili
za juu
No comments:
Post a Comment