Mazungumzo mapya yanayolenga
kumaliza mgogoro wa vita vya wenyewe kwa wenyewe wa miezi 19 Sudan
Kusini yameanza katika mji mkuu wa Ethiopia Addis Ababa.
Wapatanishi
kutoka shirika la IGAD wanajaribu kuwarai rais Salva Kiir na kiongozi
wa waasi Riek Machar kutia sahihi mkataba wa amani kufikia mwezi Agosti.Bwana Machar amesema kuwa makataa yaliowekwa ni vigumu kuyaafikia.
Baraza la makanisa lenye ushawishi mkubwa nchini humo limewataka viongozi hao wawili kusitisha vita hivyo mara moja ,likisema haikubaliki kwamba watu wanaendelea kufariki huku wao wakizozania mamlaka.
No comments:
Post a Comment