06 August, 2015

Kwamujibu wa Forbes, Hawa ndio waigizaji 10 wanaolipwa mkwanja mrefu zaidi duniani

post-feature-imageUsanii wa uigizaji katika filamu hutuacha na hisia tofuati tunapowatazama hasusan waigizaji nguli.
Lakini je, unafahamu kiasi cha fedha wanazolipwa kwa uigizaji wao ?
Jarida la Forbes limezindua orodha ya waigizaji bora na wanaolipwa mshahara wa juu zaidi duniani.
Jarida hilo limeangazia faida wanazopata baada ya kulipa gharama kama vile kodi na ada ya wasimmamizi wao. Kwa mwaka wa tatu mfululizo, muigizaji wa filamu ya Iron Man, Robert Downey Jr anaongoza orodha hiyo.

Downey Jr alitia kibindoni dola milioni $80m . Downey ameshiriki katika filamu za 'Avengers' na 'Age of Ultron'. Na kwa mara ya kwanza, orodha hiyo imewashirikisha waigizaji wanaoigiza nje ya Hollywood.

Hii inamaanisha kuwa wasanii watajika katika filamu nje ya Marekani kama vile Bollywood ya India na wasanii wa Asia pia wamejumuishwa katika orodha hiyo. Muigizaji nyota kutoka Uingereza Daniel Craig aliorodheshwa katika nafasi ya 15 sawa na Chris Hemsworth kutoka Australia.

Wawili hao walizoa takriban dola milioni $27m kwa mujibu wa Forbes. Msanii Jackie Chan wa filamu ya Karate Kid miongoni mwa nyingine nyingi tu, ameorodheshwa katika nafasi ya pili.

Chan alipokea dola milioni 50 mwaka uliopita kwa kazi yake.
Tazama Orodha kamili hapa

Hawa ndio wasanii wanaolipwa vyema kulingana na Forbes.


  1. Robert Downey Jr - $80m
  2. Jackie Chan - $50m
  3. Vin Diesel - $47m
  4. Bradley Cooper - $41.5m
  5. Adam Sandler - $41m
  6. Tom Cruise - $40m
  7. Amitabh Bachchan - $33.5m
  8. Salman Khan - $33.5m
  9. Akshay Kumar - $32.5m
  10. Mark Wahlberg - $32m

No comments:

Post a Comment

Samsung kurejesha fedha kwa wanunuzi wa Note 7

KAMPUNI ya Vifaa vya Elektoriniki ya Samsung ya Afrika Mashariki (SEEA) itarejesha fedha kwa wateja wa simu za Note 7, ambao wataweza kuthib...