
Baadhi ya wasanii na wadau wa sanaa wamesema BASATA huwa haionekani kusemea suala la hati miliki ya kazi za wasanii au kusimamia maslahi ya wasanii bali imeishia kwenye nidhamu tu.
Nuhu Mziwanda ambaye ni msanii wa muziki wa Bongo Flava na pia ni mpenzi wa Shilole naye ameamua kuandika yake baada ya mpenzi wake kufungiwa kazi za sanaa kwa mwaka mzima.
Haya ndiyo aliyo aandika Instagram.
"Hili si swala la kuchekelea au kumkejeli mtu au kueka chuki'sisi sote binadamu tunapita katika hii dunia na kila mtu ana kazi anayofanya 'tunalalamikaga kazi zetu zinaibiwa lakini hakuna hatua yoyote inayochukuliwa 'tuuze madawa ya kulevya ili tuuwawe nchi za watu,au mnataka ajiuze barabarani? na si kila afanyae kazi anapatia'kuna mda ajali zinatokea popote hata uwe unauza vitumbua vinaweza vikaungua jikoni'sisi ni Watanzania na inabidi tulichanganue hili swala ili kukuza mziki wetu mana ni tatizo kubwa sana na ni msanii mkubwa mwenye mashabiki wengi sana Africa'naomba tuungane kueka jambo sawa'Basata ni wazazi wetu na wanaelewa tunategemea sanaa kula ugali na kuendesha familia'hili swala lifikiliwe mara ya pili" Ameandika Nuhu Mziwanda.
No comments:
Post a Comment