Watu watatu wamekufa na wengine
thelathini wamelazwa hospitalini kutokana na mlipuko wa ugonjwa wa
kipindupindu nchini Tanzania na hasa katika mji wa kibiashara wa Dar es
salaam.
Wataalamu wa afya wamesema kwamba mlipuko huo unapatikana
kwenye maeneo ambayo hayana usafi wa kutosha na vyoo vya kisasa hasa
katika maeneo yenye msongamano wa makazi katika jiji hilo.Umma wa watanzania wametakiwa kuwa waangalifu baada ya kifo cha mwanamke mmoja mwenye umri wa miaka ishirini na saba,mwishoni mwa wiki iliyopita baada ya kuonesha dalili zinazoshabihiana na magonjwa ya milipuko.
Dar es salaam ni mmoja kati ya miji yenye idadi kubwa ya watu, mji huo pekee una idadi ya watu zaidi ya milioni tano.
Watu waishio katika makazi holela wako katika hatari kubwa ya kuambukizwa ugonjwa wa kipindupindu kutokana na kutokuwa na vyoo bora na vya kisasa .
BBC
No comments:
Post a Comment