KOCHA wa Simba, Dylan Kerr ametamba kikosi chake kimekamilika kila
idara na endapo atapata nafasi ya kumsajili straika mwenye rekodi nzuri,
hakuna kitakachoizuia timu yake kutwaa ubingwa wa Ligi Kuu Bara.
Kerr raia wa Uingereza hakulificha Championi Jumamosi, kwani amesema,
kila akikitazama kikosi chake anaona kimekamilika kuanzia mabeki,
viungo na hata washambuliaji lakini akagutuka kitu kidogo tu.
“Timu yangu naiona imetimia kila idara, lakini kuna kitu kimoja
kinaniumiza kichwa, nacho ni kusajili straika mmoja hatari mwenye uwezo
wa kufunga na kutoa pasi za mwisho.
“Tena huyo mchezaji nataka awe na rekodi zilizo wazi kila mmoja ajue,
siyo sifa za kuambiwa na watu! Huyo simtaki kabisa kwani hatokuwa na
jipya,” alisema Kerr kwa msisitizo.
Ili kuonyesha kwamba hana utani, Kerr alisema: “Nina majina ya mastraika
tisa kutoka nchi mbalimbali za Afrika, kati yao ni mmoja tu
nitakayemsajili baada ya kuridhika na sifa zake.”
Mastraika hao wanatokea nchi za DR Congo, Rwanda, Nigeria, Zambia, Botswana, Msumbiji, Ghana, Namibia na Afrika Kusini.
Huku akizungumza kwa umakini, Kerr alisema: “Bado naendelea kupitia
rekodi ya kila mmoja wao na kujiridhisha na uwezo wao wa kufunga mabao
kupitia Mitandao ya Wikipedia na Youtube, nikiridhika nitakuambia nani
namsajili.”
Alisema mbali ya uwezo wa kufunga na kutoa pasi za mwisho, straika
anayemuhitaji ni mwenye umri usiozidi miaka 28 kwani atakuwa bado na
uwezo wa kupambana.
“Mawakala wanaendelea kunitumia majina na video za mastraika na kazi
yangu ni kutazama yupi anafanya vizuri, halafu namchagua aliye bora kati
yao,” alisema Kerr.
Kwa sasa, safu ya ushambuliaji ya Simba inaundwa na Hamis Kiiza, Mussa
Mgosi waliosajiliwa na hivi karibuni na Ibrahim Ajib. Katika mechi sita
ilizocheza, Simba imefunga mabao 17 huku washambuliaji hao wakifunga
mabao 10. Mgosi na Kiiza wamefunga matatu kila mmoja huku Ajib akifunga
manne.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
Samsung kurejesha fedha kwa wanunuzi wa Note 7
KAMPUNI ya Vifaa vya Elektoriniki ya Samsung ya Afrika Mashariki (SEEA) itarejesha fedha kwa wateja wa simu za Note 7, ambao wataweza kuthib...
-
C9 Records presents STAR by Foby!. Click DOWNLOAD button bellow to download this song.
-
John ana mke ambaye haoni uzuri wa kitu chochote anachofanya, akifika tu nyumbani mke wake huanza kumlalamika kuwa hela anayoacha nyumba...
-
Mboga za majani na matunda zimekuwa zikisisitizwa kwa sana na wataalamu wa afya hasa kwa wanawake wajawaziti kwani zimekuwa zikiongeza Damu...
No comments:
Post a Comment