11 August, 2015

Idris Sultan amjibu Nuh Mziwanda madai kuwa anamtongoza Shilole, Haya ndiyo aliyoandika leo

Sakata la kuhaha kwa Nuh Mziwanda kuhusiana na penzi lake kwa Shilole linaweza kumsababisha akakorofishana na baadhi ya mastaa wenzake. Jana Nuh Mziwanda alicomment kwenye post ya mshindi wa BBA 2014 Indris Sultan kwakuandika kuwa hafurahishwi na kitendo chake cha kumtongoza Shilole na kumtaka aache hiyo tabia.

Lakini pia mapema leo asubuhi Mziwanda aliamka na kuandika ujumbe mzito kwa aliyekuwa Miss Tanzania 2006 Wema Sepetu kuwa anatuma team Wema kumtongoza Shilole haswa baada ya sauti iliyo sikika ya Mziwanda akimtongoza Wema kuleta shida kwenye penzi lao.

Idris Sultan ameandika haya kwenye account yake ya Instagram kuhuisiana na ujumbe wa Mziwanda kudai kuwa amekuta jumbe za maandishi kwenye simu ya Shilole zinazo onyesha niza Idris kumtongoza Shilole. Haya ndiyo aliyo andika
Kati ya vitu sisubiri kuambiwa ni ikiwemo kuwa am social. Tabia yangu ikiwemo kupenda watu na kufanya mazungumzo na wengi. Sasa unapokuja na agenda za nje kwangu nakukaribisha sio kuwa sikujui ila nakuvumilia na kukupa mda wa kujirekebisha. Kama mwanaume uliyekamilika huwezi kuja insta kiholelaholela kulalamika kuwa mwanamke wako anasumbuliwa, 1. Huna namba yangu 2. Mbona mwanamke wako hasemi 3. Ulikua unafanya nini kwenye simu yake kukagua message au na pochi unambebea 4. Naanzia wapi kumsumbua mwanamke wako, hivi umemuona wangu kwakweli ? 5. We ni mwanamziki au muuza magazeti mbona uswahili sana ?. Ukitaka kumsumbua wangu sikukatazi ila njoo na dictionary. Watu tuna amani na upendo ila vipepeo vyako vinaweza kuleta unnecessary riots. Najulikana Africa nina mashabiki wanaonipenda na walionichagua na nina ndoto zangu na zao za kutimiza ukijua levo uliyopo na levo niliyopo angalau siku ukijulikana hata kinondoni vizuri basi utajua kina nani wa kuwaheshimu na nani wa kuwapigia kelele. Shishi baby boo lovie sweetie we will support you all day everyday regardless ya wrong choice of men uliyoifanya hapa.
A photo posted by Idris Sultan (@idrissultan) on

No comments:

Post a Comment

Samsung kurejesha fedha kwa wanunuzi wa Note 7

KAMPUNI ya Vifaa vya Elektoriniki ya Samsung ya Afrika Mashariki (SEEA) itarejesha fedha kwa wateja wa simu za Note 7, ambao wataweza kuthib...