Bayern Munich walianza vyema
kutetea ubingwa wao wa Bundesliga wakiifunga 5-0 Hamburg SV kwenye mechi
iliyopigwa Ijumaa iliyopita uwanja wa Allianz Arena, huku Thomas
Muller akifunga magoli mawili.
Wakati huo huo, Manchester
United walipata ushindi wao wa pili kwa kushinda 1-0 dhidi ya Aston
Villa, ingawa bado hofu ipo katika safu yake ya ushambuliaji.
Leo gazeti la The Sunday
Express limeandika stori ukurasa wake wa nyuma akisomeka: “Thomas Muller
anataka kujiunga na Manchester United, hii ni kwa mujibu wa John
Richardson.
Sunday Express wanaonekana
kupata habari hiyo kutoka vyanzo makini vya masuala ya usajili
vinavyodai Muller anataka kujiunga na mchezaji mwenzake wa zamani wa
Bayern Munich aliyetimkia Old Trafford, Bastian Schweinsteiger.
Hata hivyo, bosi wa Man United,
Louis van Gaal bado hajakata tamaa kumfukuzia Muller, licha ya ofa yake
kukataliwa. Dau la mwisho aliloweka mezani ni paundi milioni 60.
United wataendelea kujaribu kumsajili Muller na gazeti hilo pia limesema kwamba Van Gaal anamuwinda Gareth Bale.
Tazama ukurasa wa nyuma wa Sunday Express, huku zikifuatiwa baadhi ya tweets juu ya tetesi hiyo.
No comments:
Post a Comment