14 August, 2015
Azam TV Yazindua Huduma Yake Ya “Azam Sports HD”
Azam Media leo imezindua rasmi chaneli yake mpya yenye ubora wa juu kabisa iitwayo “Azam Sports HD”, tangu kuanza kwa huduma za Azam TV, wateja wamekuwa wakijiuliza hasa ni kipi wanachopata kutokana na alama ya HD iliyo mbele ya kisimbuzi, kuanzia sasa watafahamu.
Baada ya miezi 18 ya mipango na uwekezaji, leo umeshuhudiwa uzinduzi wa channel ya kwanza itakayowezesha wateja kufaidi picha na sauti za ubora wa juu kabisa “HD” kutokana na teknolojia ya kiwango cha juu.
Wateja wa kifurushi chenye channel mpya ya “Azam Sports” wataweza kuona timu zao wazipendazo katikaVPL katika picha ang’avu zaidi ambazo hazijawahi kuonekana, zaidi, kampuni pia imetangaza rasmi ujio wa ligi kuu ya Uhispania maarufu la liga ambayo wateja wataipata katika ubora wa HD kupitia chaneli mpya.
Mchezo wa kwanza kuoneshwa katika msimu mpya wa la liga 2015/16, ni Malaga dhidi ya Seville wa Ijumaa 21 Agosti 2015 na timu zote vigogo zitakuwa zikicheza na kuonyeshwa Live mwisho wa juma lijalo, na kila mzunguko wa msimu mzima katika ubora wa HD.
Kifurushi kinachojumuisha chaneli ya Azam Sports HD kitaonekana kwa watazamaji wa Azam TV wa Tanzania pekee ambao wanalipa kifurushi chochote kati ya vitatu vya sasa, Pure, Plus au Play na nyongeza ya shilingi 15,000 kwa mwezi, ikijumuisha VAT. Pamoja na chaneli mpya ya Azam Sports HD, malipo hayo yatajumuisha chaneli za klabu za Manchester United, Liverpool na Real Madrid ambazo kwa sasa ni sehemu ya kifurushi cha Azam Play. Kadhalika malipo ya mwezi kwa kifurushi cha Play kitapunguzwa hadi 25,000 kuanzia sasa.
Kwa wale wasiokuwa na luninga zenye uwezo wa kuona picha za HD au waya maalum wa HD (HDMI), watapata chaneli mpya na kufuatilia La Liga na mengineyo – japo si kwa ubora wa HD. Pia kwa wateja wasiohitaji kujiunga na kifurushi kipya hawapaswi kuwa na wasiwasi wa kutoona michezo ya VPL kwani itaendelea kuonyeshwa kupitia Azam One na Azam Two kama ilivyokuwa kabla , jambo lililotofauti ni kuwa mchezo yenye mvuto zaidi itaonyeshwa pia kwenye Azam Sports HD.
Zaidi ya La Liga na VPL , Azam Sports HD, itakuwa na vitu mbalimbali vya kimichezo vitakavyojumuisha michezoya Ligi za soka za Uganda, Kenya na Burundi itakayoanza hivi hivi karibuni.
Akizungumza wakati wa hafla ya uzinduzi, Afisa Mtendaji Mkuu wa Azam Media, Rhys Torrington amesema “Uzinduzi wa Azam Sports HD ni hatua kubwa katika maendeleo ya Azam TV. Hata kabla ya ya kuanza mwaka 2013 tulijipanga kukidhi mahitaji ya kiteknolojia kwa ajili ya kutoa picha za ubora wa HD ili kutuwezesha baadaye kumpatia mtazamaji picha bora zaidi bila kulazimika kununua vifaa kwa kuonyesha moja kwa moja soka la Liga! Ambalo ni bora zaidi barani Ulaya”.
Uwezo wa kuona moja kwa moja na katika HD timu mzipendazo huko Hispania na kwa VPL , pamoja na vipindi vingine vya michezo kutoka sehemu mbalimbali duniani, unatoa chaguo muhimu na ambalo wateja wetu wanalimudu, huu ni mwanzo tu – jiandae kwa makubwa zaidi”.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
Samsung kurejesha fedha kwa wanunuzi wa Note 7
KAMPUNI ya Vifaa vya Elektoriniki ya Samsung ya Afrika Mashariki (SEEA) itarejesha fedha kwa wateja wa simu za Note 7, ambao wataweza kuthib...
-
C9 Records presents STAR by Foby!. Click DOWNLOAD button bellow to download this song.
-
John ana mke ambaye haoni uzuri wa kitu chochote anachofanya, akifika tu nyumbani mke wake huanza kumlalamika kuwa hela anayoacha nyumba...
-
Mboga za majani na matunda zimekuwa zikisisitizwa kwa sana na wataalamu wa afya hasa kwa wanawake wajawaziti kwani zimekuwa zikiongeza Damu...
No comments:
Post a Comment