31 July, 2015

OLYMPIC GAMES: NI BEIJING TENA 2022

001ec94a26ba0a1c636309
Wakati Urusi ikijiandaa kuandaa mashindano ya kombe la dunia mwaka
2018, marafiki wa Urusi kisiasa nchi ya China, imechaguliwa kuandaa
mashindano mengine makubwa duniani ya Olympic mwaka 2022. Jiji la
Beijing ndio limechaguliwa kuandaa mashindano hayo kwa mara nyingine
tena kwani mwaka 2008 pia walipata nafasi hiyo.
Beijing itafanya hivyo kwa mara nyingine huku ikiwa ya kwanza kuandaa
mashindano hayo nyakati zote mbili {majira ya baridi na kiangazi}.
Beijing ililishinda jiji la Almaty la nchini Kazakhstan.
Mashindano ya Olympic yaliyopita nchini china yalilaumiwa kutokana na
hali ya hewa kutokuwa nzuri, hata hivyo kamati ya maandalizi ya
michuano hiyo imedai mashindano yajayo yatakuwa bora Zaidi pengine
kuliko mashindano yoyote yaliyo wahi kufanyika.
Beijing ilipata kura 44 dhidi yakura 40 za Almaty, Thomas Bach rais wa
kamati ya Olympic alitangaza matokeo hayo mapema leo Ijumaa.

No comments:

Post a Comment

Samsung kurejesha fedha kwa wanunuzi wa Note 7

KAMPUNI ya Vifaa vya Elektoriniki ya Samsung ya Afrika Mashariki (SEEA) itarejesha fedha kwa wateja wa simu za Note 7, ambao wataweza kuthib...