09 July, 2015

Mchezaji raia wa Ureno, Luis Almeida da Cunha ‘Nani’ ametuma ujumbe mzito wa kuiaga klabu yake ya zamani Manchester United.

nani

Luis Nani ambaye alikua kwa mkopo wa msimu mzima nyumbani kwao na klabu ya Sporting Lisbon, amekamilisha uhamisho wa pauni 3.5m kujiunga na Fernabache ya Uturuki.
Kupitia ukurasa wake wa Instagram, Luis Nani ameandika maneno ya moyoni kuhusu maisha yake ya soka hususani na klabu ya Manchester United na ujumbe huo ni mahususi usomwe na mashabiki wa Manchester united.
Pamoja na kuwashukuru mashabiki, wachezaji wenzake, benchi la ufundi pamoja na wote waliomsaidia kufika hapo alipo, lakini Nani ametoa salamu za pekee za shukrani kwa aliyekuwa kocha wa klabu hiyo Sir Alex Ferguson.
Alex Ferguson ambaye alimsajili Nani kwa pauni 17m alistaafu kufundisha soka mwaka 2013 na kuacha maisha ya Luis Nani utatani.
Akiwa United, Luis Nani ameshinda makombe 4 ya ligi kuu, kombe la ligi yaani Capital One Cup, klabu bingwa Ulaya pamoja klabu bingwa ya dunia.
Winga huyo pia katika michezo 230 aliyoichezea klabu ya Manchester United, alifanikiwa kufunga magoli 40.
Pamoja na kutokuwa na fomu nzuri chini ya kocha David Moyes, lakini hali ilikua ni mbaya zaidi baada ya ujio wa kocha Louis Van Gaal ambaye alipofika tu aliamua kumtoa kwa mkopo wa mwaka mzima nchini Ureno (Sporting Lisbon) kabla ya kumuuza wiki hii katika klabu ya Fernabache.
nani
nani2
Usisumbuke Mawerenewz.blogspot.com ndio mtandao wako wakipekee unaokupa habari za BURUDANI,MICHEZO, SIASA, na HABARI MBALIMBALI ZA KIMATAIFA pamoja na KITAIFA Endelea kutembelea MTOKA MBALI pia nifuate twitter>>>@mawere3, facebook>>>Mawere Mtoka Mbali, Instagram>>>mawere_mtoka_mbali,

No comments:

Post a Comment

Samsung kurejesha fedha kwa wanunuzi wa Note 7

KAMPUNI ya Vifaa vya Elektoriniki ya Samsung ya Afrika Mashariki (SEEA) itarejesha fedha kwa wateja wa simu za Note 7, ambao wataweza kuthib...