Utata kuhusiana na sakata zima la taarifa za Nuh Mziwanda kumtia mimba
mchepuko, na kusababisha vita kali kati yake na Shilole ambaye ni mpenzi
wake, limepatiwa ufumbuzi usiku wa jana katika show kali ya burudani ya
Friday Night Live.Kama ulipitwa, picha zima kuhusiana na sakata hili lilianza kwa
Nuh
kutolea ufafanuzi kashfa hiyo inayomkabili, akidai anampenda sana Shishi
wake.
Baada ya Nuh kusepa, exclusively FNL wakamleta mbele ya Afrika Mashariki
Rose, Mchepuko aliyedai kuwa na mimba ya msanii huyo ambaye licha ya
kupotezea suala zima la kuwa na ujauzito, ambapo alikana kuwa na mimba
ya msanii huyo, lakini kukiri kuwa anampenda na wamewahi kukutana
kimwili, "ku-do", ama kufanya mapenzi katika siku za hivi karibuni bila
ya Shilole kujua.
Picha halikuishia hapo, Maelezo haya yakamfanya Shilole kutoka huko
alipokuwa na kumchukua Nuh na kurejea naye katika show, uso kwa uso na
mchepuko wa baby wake, Rose ambaye mbele ya Afrika Mashariki na mbele ya
Nuh na Shilole akasema kuwa suala la kutangaza kuwa ana mimba ni la
uongo na alisema kwa hasira baada ya Shilole kumshambulia na kumuumiza
baada ya kumkuta akiwa karibu na Nuh Mziwanda, na baada ya hapo kuwaomba
radhi wapenzi hao kwa usumbufu aliowasababishia.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
Samsung kurejesha fedha kwa wanunuzi wa Note 7
KAMPUNI ya Vifaa vya Elektoriniki ya Samsung ya Afrika Mashariki (SEEA) itarejesha fedha kwa wateja wa simu za Note 7, ambao wataweza kuthib...
-
C9 Records presents STAR by Foby!. Click DOWNLOAD button bellow to download this song.
-
John ana mke ambaye haoni uzuri wa kitu chochote anachofanya, akifika tu nyumbani mke wake huanza kumlalamika kuwa hela anayoacha nyumba...
-
Mboga za majani na matunda zimekuwa zikisisitizwa kwa sana na wataalamu wa afya hasa kwa wanawake wajawaziti kwani zimekuwa zikiongeza Damu...
No comments:
Post a Comment