Msanii huyo ambaye ni mzaliwa wa Uingereza aliyejenga jina lake kwa
kuigiza katika filamu ya Dracula na Frankenstein katika filamu ya
kutisha aligiza katika zaidi ya filamu 250.Alijulikana sana kwa kuigiza kama Scaramanga katika filamu ya James Bond
na Evil Wizard Suriman katika filamu ya Lord of the Rings.
Msanii huyo pia ameigiza katika filamu za The Wicker Man na Stars wars.
Inaripotiwa kuwa mwigizaji huyo alifariki siku ya jumapili katika hospitali ya Chelsea Westminster mjini London baada ya kulazwa na ugonjwa wa tatizo la mapafu na moyo.
No comments:
Post a Comment