23 June, 2015

Dylan Kerr kocha mpya wa Simba, anatokea Uingereza

Hatimaye kocha mpya atakayeanza kukinoa kikosi cha wekundu wa Msimbazi, Simba Sports Club, amefahamika.Kocha huyo ambaye ni raia wa Uingereza, anaitwa Dylan Kerr na tayari ameingia makubaliano na uongozi wa Simba kuanza kazi hiyo kwenye msimu ujao wa ligi kuu ya Tanzania bara
.Kerr atachukua nafasi ya Goran Kopunivoc ambaye mkataba wake umemalizika. Kopunivoc alimaliza mkataba wake kwa kushika nafasi ya tatu kwenye ligi kuu iliyomalizika.Kocha huyo mpya wa Simba ataingia nchini wiki hii.
Akitua Tanzania kocha huyo atatambuliswa rasmi mbele ya waandishi wa habari.
Pamoja na Muingereza huyo, Simba pia imemtangaza kocha mpya wa makipa, Abdul Idd Salim kutoka Kenya.

No comments:

Post a Comment

Samsung kurejesha fedha kwa wanunuzi wa Note 7

KAMPUNI ya Vifaa vya Elektoriniki ya Samsung ya Afrika Mashariki (SEEA) itarejesha fedha kwa wateja wa simu za Note 7, ambao wataweza kuthib...