10 June, 2015

alichokisema Chris Brown kuhusu mapenzi yake na Karrueche..

Story kubwa nyingine ikachukua headlines, washkaji wa Chris Brown walipanga mchezo marafiki wa kuwakutanisha pamoja wakijifanya eti Karrueche alitaka kukutana na Chris Brown ili kumaliza tofauti zao na kuendelea na uhusiano.

Chris Brown akapata airtime ya interview iHeart Radio, moja ya maswali yaliyoulizwa ni kama anampenda Karrueche?
“Siwezi kuahidi chochote kwa sasa kwani sitaki kukurupuka, ndio bado nampenda sana siwezi kudanganya.. ila katika maisha inafika wakati inabidi tusimame tuangalie mapungufu.
“tusonge mbele na tutafute namna ya kutatua matatizo hayo… nakubali kuwa nilikosea na inabidi sasa nisimame kutazama nilipokosea kipindi cha nyuma …mimi ni baba sasa … kuhusu mimi na yeye, tuipe muda.”
Ameongelea pia kuhusu mtoto wake wa mwaka mmoja Royalty na maisha ya kuwa baba pamoja na magari na anayotembelea.
Msikilize Chris Brown kwenye Interview hiyo hapa mtu wangu.

No comments:

Post a Comment

Samsung kurejesha fedha kwa wanunuzi wa Note 7

KAMPUNI ya Vifaa vya Elektoriniki ya Samsung ya Afrika Mashariki (SEEA) itarejesha fedha kwa wateja wa simu za Note 7, ambao wataweza kuthib...