07 May, 2015

Yaya Toure kuihama Manchester City.

YAYA_TOURE
Huku msimu wa ligi ukiwa si wa mafanikio kwa Manchester City baada ya klabu hiyo kushindwa kutetea taji lao la ligi kuu ya England ambalo walitwaa msimu uliopita na pia wakishindwa kwenda mbele kwenye michuano ya ligi ya mabingwa baada ya kutolewa kwenye hatua ya 16 bora , hali imezidi kuwa
mbaya kwa Manchester City baada ya taarifa za kuondoka kwa kiungo wake wa kutegemewa Yaya Toure kuibuka .
Wakala wa kiungo wa Ivory Coast Yaya Toure Dimitri Seluk amevithibitishia vyanzo mbalimbali vya habari hii kuwa mteja wake ana asilimia 90% ya kuihama klabu hiyo baada ya kumalizika kwa msimu huu .
Wakala huyo amefichua kuwa uhusiano wa Yaya na Manchester City umekuwa mbovu na imefikia hatua mbaya kiasi cha mchezaji huyo kufanya maamuzi ya kuondoka na kufikia uamuzi ambao hawezi kuubadilisha .
Itakumbukwa kuwa Kiungo huyo aliingia kwenye ugomvi ambao uliripotiwa sana kwenye vyombo vya habari mwaka jana wakati klabu yake iliposhindwa kumfanyia hafla ya siku yake ya kuzaliwa wakati City ilipokuwa kwenye ziara ya huko Falme Za Kiarabu ripoti ambazo baadae zilikanushwa.Yaya Toure amehusishwa na kuungana na kocha wake wa zamani Roberto Mancini anayefundisha klabu ya Inter Milan .
Wakati hayo yakiendelea Yaya Toure kwa nyakati kadhaa wamekuwa akihusishwa na mpango wa kujiunga na kocha wake wa zamani Roberto Mancini ambaye kwa sasa anaifundisha Inter Milan .
Kwa upande wa uongozi wa Man City inasemekana kuwa klabu hiyo inajiandaa kusikiliza ofa zitakazokuja kwa ajili ya mchezaji huyo kutokana na umri wake kusogea huku uongozi ukiwa na mpango wa muda mrefu wa kujenga kikosi cha City kwa kuwategemea zaidi wachezaji wenye umri mdogo .

Mawerenewz.blogspot.com ndio mtandao wako wakipekee unaokupa habari za BURUDANI,MICHEZO,SIASA, na HABARI MBALIMBALI ZA KIMATAIFA pamoja na KITAIFA Endelea kutembelea MTOKA MBALI pia nifuate twitter>>>@mawere3, facebook>>>Mawere Mtoka Mbali, Instagram>>>Zawadi_mawere. Youtube>>>MAWERE TV.

No comments:

Post a Comment

Samsung kurejesha fedha kwa wanunuzi wa Note 7

KAMPUNI ya Vifaa vya Elektoriniki ya Samsung ya Afrika Mashariki (SEEA) itarejesha fedha kwa wateja wa simu za Note 7, ambao wataweza kuthib...