17 May, 2015

UONGOZI wa Simba umethibitisha rasmi kuachana na aliyekuwa kocha mkuu wake,

_MGM6121
UONGOZI wa Simba umethibitisha rasmi kuachana na aliyekuwa kocha mkuu wake, Mserbia Goran Kopunovic baada ya kushindwa kufikia makubaliano juu ya mkataba mpya.
Mwenyekiti wa kamati ya usajili ya Simba, Zacharia Hans Poppe amesema Kopunovic ameshuka kidogo mno kwenye dau alilotaka na
Simba wameshindwa kufikia uwezo huo.
“Amebaki palepale, ameshuka kidogo sana, tumeona atafute maslahi ya namna hiyo kwenye timu nyingine, sisi hatuwezi kufikia. Unaweza kusema hakushuka kabisa, yaani katika hela zote alizotaja ameshuka kwa dola elfu tano tu”. Amesema Hans Poppe na kuongeza: “Tumeshaona makocha karibu sita kutoka Serbia, Hungary, Bulgaria na Burundi pia tunaangalia, kuna kocha ambaye CV zake ni nzuri”.
Goran Kopunovic 
Hans Poppe ameongeza: “Hatudaiani na Kopunovic, mkataba wake umekwisha. Mrithi wa Goran ndani ya wiki moja tutakuwa tumempata. Atakakuja kocha tu, wasaidizi wataendelea walewale, hatukupenda kubadilisha, lakini bahati mbaya tumeshindwa kuafikiana, amekwenda juu mno tofauti na matarajio yetu, tungependa kuendelea na Kopunovic, ni kocha mzuri, ameifundisha timu vizuri”.
Kopunovic alitaka mshahara mkubwa wa dola za Kimarekani elfu tisa (9,000) sawa na shiloingi milioni 18 za Kitanzania.
Pia anataka dau la kusaini la dola za kimarekani elfu hamsini (50,000) sawa na shilingi million 100 za Kitanzania.
Taarifa zilizoripotiwa jana ni kwamba kocha Mbelgiji, Piet de Mol atatua Dar es Salaam Mei 21, mwaka huu kwa ajili ya mazungumzo ya kuifundisha Simba SC.
Kwa mujibu wa mtandao wa Wikipedia, De Mol mwenye umri wa miaka 60 ana uzoefu mkubwa wa kufundisha soka Afrika, Asia na Ulaya na alikuwa nchini Ghana akifanya kazi ya Mkurugenzi wa Ufundi wa akademi mjini Kumasi. Pia alifanya kazi na Asante Kotoko. Pia alifundisha timu ya kwao Ubelgiji, Dubai, Qatar na China. Alikuwa kocha Msaidizi wa AA Gent kuanzia mwaka 1997 hadi 2001.
Naye kopunovic leo akiwa Hungary amethibitisha kushindwana na Simba, lakini amedai kuwa atakuwa shabiki mkubwa wa timu hiyo kwani hakupenda kuondoka.
Simba imekosa kushiriki michuano ya kimataifa kwa miaka mitatu, kwa mara ya mwisho ni mwaka 2012 walipotwaa ubingwa wa Tanzania.
Moja ya sababu kubwa Simba kuchemsha katika michuano ya ligi kuu ni mabadiliko ya mara kwa mara ya makocha.
Toka walipochukua ubingwa 2011/2012 chini ya kocha Maserbia Milovan Circovic, Simba imepitia mikononi mwa Mfaransa Patrick Liewig, Mzawa Abdallah Kibadeni, Mcroatia, Zdravko Logarusic, Mzambia Patrick Phiri na sasa wameachana na Mserbia, Goran Kopunovic.

Mawerenewz.blogspot.com ndio mtandao wako wakipekee unaokupa habari za BURUDANI,MICHEZO, SIASA, na HABARI MBALIMBALI ZA KIMATAIFA pamoja na KITAIFA Endelea kutembelea MTOKA MBALI pia nifuate twitter>>>@mawere3, facebook>>>Mawere Mtoka Mbali, Instagram>>>mawere_mtoka_mbali,SuScribe Youtube>>>MAWERE TV



No comments:

Post a Comment

Samsung kurejesha fedha kwa wanunuzi wa Note 7

KAMPUNI ya Vifaa vya Elektoriniki ya Samsung ya Afrika Mashariki (SEEA) itarejesha fedha kwa wateja wa simu za Note 7, ambao wataweza kuthib...