LUKAS Podolski, mshindi wa
kombe la dunia akiwa na timu ya taifa ya Ujerumani mwaka jana nchini
Brazil ambaye kwasasa yupo kwa mkopo Inter Milan kutokea Arsenal
amehojiwa kuhusu mtoto wake na kufichua kuwa anazivutia klabu nyingi.
Mtoto huyo mwenye miaka 7
anayeitwa Louis Podolski, kwasasa yupo katika kituo cha watoto cha
Bambini cha Inter na Podolski ametangaza kuwa klabu tatu za Ujerumani
zinajaribu kuiwinda saini ya mtoto wake ili ajiunge na timu zao za
vijana.
Timu hizo ni Cologne, Bayer Leverkusen na Borussia Mönchengladbach.
Podolski amesema: “Mtoto wangu sasa ana miaka 6 kuelekea saba, anaichezea Bambini (Inter). Tayari ameshanasa kwenye rada. Sasa Cologne, Leverkusen na Gladbach wanahitaji kumsajili. Katika umri huu, inashangaza!”
Podolski alijiunga kwa mkopo na
Inter katika dirisha dogo la usajili mwezi januari mwaka 2014 na
anatarajia kurejea Arsena mwishoni mwa msimu huu.
No comments:
Post a Comment