Taarifa kutoka chanzo cha
kuaminika ndani ya klabu ya Azam fc zinaeleza kuwa kocha wa zamani wa
klabu hiyo, Muingereza Stewart John Hall anarejea tena kuwa kocha mkuu.
Hall aliyeiacha Azam fc baada ya
kumalizika kwa mzunguko wa kwanza wa ligi kuu msimu wa 2013/2014
anarejea kuchukua mikoba ya aliyekuwa kocha mkuu, Joseph Marius Omog.
Omog alifukuzwa kazi mwezi
februari mwaka huu baada ya Azam kutolewa ligi ya mabingwa Afrika na El
Merreick kwa ushindi wa jumla wa magoli 3-2 na nafasi yake ikachukuliwa
kwa muda na aliyekuwa kocha msaidizi, George ‘Best’ Nsimbe.
Kwasasa Nsimbe ndiye kocha mkuu
wa muda na msaidizi wake ni Dennis Kitambi, hivyo kurejea kwa Hall kuna
maanisha kocha mmoja anaweza kuwa msaidizi wake.
Nsimbe ameshindwa kutetea ubingwa aliochukua Omog msimu uliopita.
No comments:
Post a Comment