SEPP BLATTER ameshinda kwa mara
ya tano kiti cha Urais wa Shirikisho la soka duniani FIFA baada ya
kupata kura 133 dhidi ya 73 za mpinzani wake Prince Ali bin Al-Hussein
katika raundi ya kwanza ya uchaguzi mkuu uliomalizika usiku huu mjini
Zurich, Uswizi.
Blatter mwenye miaka 79 alipata ushindi katika raundi ya kwanza na kabla ya kwenda raundi ya pili, Prince Ali alijitoa.
Baada ya kushindwa katika
uchaguzi huo, Prince Ali amesema: “Nashukuru nyote. Imekuwa safari ndefu
na ya kushangaza. Asanteni kwa wote mliopnipigia kura”
Changamoto aliyonayo Blatter ni
kukabiliana na Skendo ya rushwa ya dola milioni 100 inayowakabili
maafisa sita wa ngazi ya juu wa FIFA.
No comments:
Post a Comment