11 May, 2015

MTAZAMO WA RONALDO DE LIMA

de lima
Mshambuliaji hatari wa zamani wa Brazil Ronaldo de Lima amesema anaamini kunaupungufu mkubwa wa wachezaji wenye ubora wa hali ya juu ukiwaacha wachezaji hawa watatu kutoka Barcelona na Real Madrid,
Ronaldo na Messi ndio wachezaji wawili pekee ambao wamekua wakishinda tuzo ya mchezaji bora wa dunia kwa miaka saba mfululizo wakati Neymar amekua akitabiliwa kufanya hivyo baadae.

Hata hivyo Ronaldo ambae amechezea vilabu vyote amesema anaamini kuna pengo kubwa kati ya hawa wachezaji wa tatu na wachezaji wengine waliobakia.
Kama Zinedine Zidane alivyosema,”Nadhani messi ni wa ajabu, Ronaldo ni bora sana na Neymar pia ni wa ajabu lakini nadhani dunia ya soka inakosa baadhi ya nyota , ” alinukuliwa

Mchezaji huyo wa zamani mwenye umri wa miaka 38 amesema hataki kumfuata mchezaji mwezake wa zamani Zidane na kufanya kazi ya ukocha
“Ni rafiki wangu mkubwa kila siku tunaongelea kuhusu soka .yeye saivi ni mwalimu lakini mimi sitaki kuwa hivyo.
Presha ipo pale pale japokua wewe si ambae unaingia uwanjani na kucheza”alimaliza


Mawerenewz.blogspot.com ndio mtandao wako wakipekee unaokupa habari za BURUDANI,MICHEZO, SIASA, na HABARI MBALIMBALI ZA KIMATAIFA pamoja na KITAIFA Endelea kutembelea MTOKA MBALI pia nifuate twitter>>>@mawere3, facebook>>>Mawere Mtoka Mbali, Instagram>>>Zawadi_mawere. SuScribe Youtube>>>MAWERE TV.


1.

No comments:

Post a Comment

Samsung kurejesha fedha kwa wanunuzi wa Note 7

KAMPUNI ya Vifaa vya Elektoriniki ya Samsung ya Afrika Mashariki (SEEA) itarejesha fedha kwa wateja wa simu za Note 7, ambao wataweza kuthib...