GORAN Kopunovic bado
anaihangaisha Simba kuhusu kusaini mkataba mpya na aliahidi kutoa jibu
jana ijumaa, lakini bado amekuwa mgumu kuweka wazi kama amekubali au la!
kuendelea na kibarua chake Msimbazi.
Sababu inayofanya Simba
washindwane na Kopunovic mpaka sasa ni Mserbia kutaka mshahara mkubwa
wa dola za Kimarekani elfu tisa (9,000) sawa na shiloingi milioni 18 za
Kitanzania.
Pia anataka dau la kusaini la dola za kimarekani elfu hamsini (50,000) sawa na shilingi million 100 za Kitanzania.
Siku za karibuni, mwenyekiti wa
kamati ya usajili ya Simba, Zacharia Hans Poppe alikaririwa na vyombo
vya habari akisema wanasubiri maamuzi ya Kopunovic ambaye kwasasa yuko
likizo Hungary na kama atakataa kukubali ofa yao basi watatafuta kocha
mwingine kurithi mikoba yake.
Hans Poppe na viongozi wenzake
kwa siku nzima ya jana walikuwa wanasubiri jibu la Kopunovic, lakini
mpaka usiku hakukuwa na taarifa yoyote kutoka kwa kocha huyo mwenye
mbwembwe nyingi anapoiongoza timu yake.
Hata hivyo taarifa mpya iliyotolewa na Bin Zubeiry asubuhi ya leo inasema kocha Mbelgiji, Piet de Mol atatua
Dar es Salaam Mei 21, mwaka huu kwa ajili ya mazungumzo ya kuifundisha
Simba SC, lakini kutua kwa kocha huyo kutategemea na msimamo wa mwisho
wa Simba SC juu ya Goran.
Kwa mujibu wa mtandao wa Wikipedia,
De Mol mwenye umri wa miaka 60 ana uzoefu mkubwa wa kufundisha soka
Afrika, Asia na Ulaya na alikuwa nchini Ghana akifanya kazi ya
Mkurugenzi wa Ufundi wa akademi mjini Kumasi. Pia alifanya kazi na
Asante Kotoko. Pia alifundisha timu ya kwao Ubelgiji, Dubai, Qatar na
China. Alikuwa kocha Msaidizi wa AA Gent kuanzia mwaka 1997 hadi 2001.
No comments:
Post a Comment