Louis van Gaal anaamini msimu ujao Man United itachuana na Chelsea kuwania ubingwa
Louis
van Gaal anaamini msimu ujao Manchester United itapambana vikali na
mabingwa watarajiwa wa ligi kuu England, Chelsea katika mbio za ubingwa
baada ya kukamalisha maandalizi yake ya kabla ya msimu (pre-season)
yatayofanyika katika ziara ya Marekani.
Van
Gaal alikosoa ziara ya Marekani ambayo tayari ilikuwa imepangwa kabla
ya kuanza kazi yake majira ya kiangazi mwaka jana na kwa muda usiozidi
wiki mbili aliiongoza klabu kwenda Los Angeles, Washington DC, Detroit,
na Miami.
Ingawa
United walishinda mechi zote za maandalizi ya msimu, Mholanzi huyo
alilaumu ratiba mbaya na waliporudi England Agosti 28 kuanza ligi kuu
walivuna pointi 13 tu katika mechi 10 za kwanza.Miamba ya ligi kuu England itacheza na Club America, San Jose Earthquakes, Barcelona na PSG katika maandalizi ya kabla ya msimu
No comments:
Post a Comment